Joe Biden Afanya Mawasiliano Na Washauri Wa Usalama

 

Rais mteule wa Marekani Joe Biden amekutana na washauri wake wa usalama wa taifa katika mkutano ambao haukuhudhuriwa na wataalam wa upelelezi wa serikali, wakati rais Donald Trump anaendelea kuzuia mchakato wa kipindi cha mpito.

Biden na makam wake Kamala Harris wamejadili kuhusu maswala mbali mbali ulimwenguni katika mkutano huo na maafisa wa ujasusi na wataalam wa ulinzi.

Kati ya waliohudhuria mkutano huo ni aliyekuwa naibu wa waziri wa mambo ya nje Tony Blinken, waliokuwa mabalozi wa Marekani Nicholas Burns na Samantha Power; generali mstaafu Stanley McChrystal, miongoni mwa wengine.

Katika siku za karibuni, Wabunge kadhaa wa chama cha Republican wamesema kwamba maafisa ujasusi wa serikali, wanastahili kutoa taarifa hizo kwa Biden, kuelekea Januari 20, siku ambayo anatarajiwa kuapishwa.

Rais Donald Trump ameendelea kudai kwamba alishinda uchaguzi mkuu wa Nov 3 na kwamba kulifanyika udanganyifu katika uchaguzi huo, bila kutoa Ushahidi wowote.

Kesi kadhaa ambazo amewasilisha mahakamani kupinga matokeo hayo ya uchaguzi, zimetupiliwa mbali kwa kukosa Ushahidi.


EmoticonEmoticon