Joe Biden Anasema Trump Anatuma Ujumbe Mbaya Sana Duniani

 

Rais mteule wa Marekani Joe Biden amelaani kitendo cha Donald Trump kukubali kuwa ameshindwa katika uchaguzi wa rais, amesema kuwa 'anatuma ujumbe mbaya sana kuhusu Marekani'.

Bwana Biden amesema, alikuwa na uhakika kuwa bwana Trump alikuwa anajua kuwa hasingeshinda na kila kitu kilionekana wazi , kwa kuwa alikuwa hajitumi kabisa katika majukumu yake.

Alikuwa akiongea katika mkutano wa simu na magavana , wakiwemo wa Democrats na Republicans, kuhusu janga la corona.

Alihojiwa kuhusu suala la Trump kutokubali ushindi wake, Biden alisema rais anatuma ujumbe wa kutisha... kwa dunia nzima kuhusu jinsi demokrasia inavyofanya kazi, na hilo anapaswa kulikumbuka kwa kuwa amekuwa rais ambaye hawajibiki katika historia ya Marekani."

"Ni suala gumu kufahamu jinsi mtu anavyofikiri ," aliongeza: "Jambo ambalo analifanya linaleta hasira."

Matokeo ya uchaguzi wa rais, rais mteule huyo kutoka Democratic anaapishwa kuingia madarakani mwezi Januari.


EmoticonEmoticon