Joe Biden Avunja Rekodi Ya Obama Kwa Upataji Wa Kura Nyingi Kwenye Uchaguzi

Mgombea Urais wa Marekani Joe Biden amevunja rekodi iliyoshikiliwa na Barack Obama kwa kupata kura zaidi ya milioni 70.

Rais Barack Obama alipata kura 69,498,516 zilizoweza kumuweka madarakani mwaka 2008 kwa kuwa aliweza kuwa na 52.93% dhidi ya mpinzani wake.

Katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 Joe Biden hadi sasa amepata jumla ya kura 72,077,099 ambayo ni 50.4% dhidi ya mpinzani wake, Donald Trump mwenye kura 68,600,884 sawa na asilimia 48.


EmoticonEmoticon