Joe Biden Azungumza Na Wananchi Akielekea Kwenye Kilele Cha Ushindi, Uvumilivu Bado Unahitajika

 

Mgombea wa Urais kwa tiketi ya chama cha Democratic, Joe Biden amezungumza na umma wa Wamarekani na kutahja tena vipaumbele vyake katika kipindi hiki akiashiria ushindi wa urais. 

Pamoja na kusema zoezi la kuhesabu kura halijakamilika lakini mgombea wa urais wa chama cha Democratic  Joe Bide amesema hatua ya ushindi inayoashiria ndio inafungua njia ya zingatio la kubaliana na janga la corona, ubaguzi na mabadiliko ya tabia nchi miongoni mwa mambo mengine. 

Mgombea huyo ameyasema hayo wakati kumekuwa na ishara ya ushindi katika majimbo muhimu, wakati kwa upande wa mpinzani wake akiendelea kulalamikia kuchezewa rafu, na kutaka majimbo hayo kusimamisha zoezi la kuhesabu kura. 

Mpaka wakati huu Biden anahitaji kura sita za wajumbe wa majimbo ilikufikia 270 inayohitajika kumuingiza Ikulu.

Katika jimbo la Arizona  ambako asilimia 94 za kura zimehesabiwa Biden ana asalimia 49.9 na Trump asilimia 48.6. 

Pennsylavania ambako wapo katika asilimia 96 Trump ana asilimia 49.2 na Biden 49.5.  Georgia ambako kumehisabiwa kwa asilimia  99 Biden ana asilimia   49.5  na Trump,  49.4 North Carolina kushahesabiwa asilimia  98 na Trump kapata asilimia 50.0  Biden ikiwa  48.6, Nevada asilimia  93 Trump kapata  48.0  na Biden  49.8.


EmoticonEmoticon