Kansela Angela Merkel Aonyesha Wasi wasi Juu Ya Utolewaji Sawa Wa Chanjo Ya COVID-19

 

Viongozi wa nchi za G20 wamesema watafanya kila linalowezekana kuhakikisha usambazaji sawa wa chanjo ya virusi vya corona, lakini Kansela Angela Merkel ameonyesha wasiwasi juu ya mchakato huo kwenda taratibu. 

Katika mkutano wa kilele wa siku mbili ulioandaliwa na Saudi Arabia na kufanyika kwa njia ya vidio, mataifa tajiri zaidi ulimwenguni yaliahidi rasilimali ili kusaidia kushughulikia janga la virusi vya corona na kuunga mkono mataifa maskini ambayo uchumi wake umeathiriwa vibaya na mgogoro huo.

Kansela Merkelamesema ana wasiwasi kwamba hakuna makubaliano makubwa ya chanjo ambayo yamefikiwa na mataifa maskini hata wakati nchi tajiri zikinunua dozi kubwa kutoka makampuni ya dawa.

"Sasa tutazungumza na kundi la muungano wa chanjo ya dunia GAVI juu ya lini mazungumzo haya yataanza, kwasababu nina wasiwasi kwamba hakuna jambo lililofanyika. 

Wakati pesa ikiwepo yote basi tutaona na Ujerumani mara chache huwa haifanyi kitu lakini Ujerumani haiwezi kuunga mkono jumuiya ya kimataifa peke yake", alisema Merkel.

Kauli yake imekuja wakati mataifa tajiri yakiahidi kushughulikia mahitaji ya kifedha kuunga mkono uzalishaji na usambazaji sawa wa chanjo ya COVID-19, matibabau na vipimo. 

Katika mkutano na waandishi wa habari waziri wa mambo ya nje wa Saudi Arabia Mohammed al-Jadaan alisisitiza kuwa kulikuwa na maafikiano miongoni mwa kundi hilo la G20 akiongeza kuwa hakuna nchi itakayoachwa nyuma.


EmoticonEmoticon