Aliyekuwa
kiongozi wa wanamgambo katika taifa la jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 'Ntabo Ntaberi' amehukumiwa kifungo cha maisha jela kwa makosa ya uhalifu dhidi ya binadamu
ikiwemo ubakaji wa watu wengi.
Mahakama
ya kijeshi ilimpata Ntabo Ntaberi na hatia ya muaji, ubakaji, utumwa wa kingono
na kuwasajili watoto walio chini ya miaka 15 katika jeshi lake.
Uamuzi
huo ulitolewa baada ya kusikilizwa kwa kesi hiyo iliochukua takriban miaka
miwili ambapo waathiriwa 178 walitoa ushahidi wao.
Umoja wa
Mataifa unasema kwamba umauzi huo umeonesha 'uzoefu wa kutenda uhalifu bila
kujali una kikomo chake'.
'Uamuzi
huo unawapatia matumaini waathiriwa wa mzozo huo wa DRC , mateso waliopitia
yamesikilizwa na kutambuliwa', alisema Leila Zerrougui , mkuu wa ujumbe wa
amani wa Umoja wa Mataifa uliopo nchini DR Congo.
Ntaberi
anayejulikana kama Sheka , alikuwa mmoja wa viongozi wa kundi moja la
wapiganaji kwa jina Nduma of Congo{NDC} ambalo lilifanya operesheni zake katika
mkoa wa mashariki wa Kivu.
Eneo la mashariki mwa DRC limezongwa na mizozo , iliochochewa na migawanyiko ya kisiasa mbali na utajiri wa raslimali katika eneo hilo.
EmoticonEmoticon