Kiwango Cha Madini Ya Uranium Cha Iran Kimepita Mara 12 Ya Kiwango Kinachohitajika

 

Iran sasa ina zaidi ya mara 12 ya kiwango cha urutubishaji wa uranium chini ya mkataba wa nyuklia wa mwaka 2015 na mataifa yenye nguvu, limesema shirika hilo la dunia la udhibiti wa nyuklia.

Shirika la Kimataifa la nishati ya atomiki (IAEA) limesema kuwa akiba ya uranium ya kiwango cha chini imefikia kilo 2,442.9 mwezi huu.

Iran inasisitiza kuwa mipango yake ya nyuklia ni ya malengo ya amani tu. IAEA pia ilisema kuwa maelezo ya Iran kwa ajili ya uwepo wa nyuklia katika eneo ambalo haijalitangaza wazi ''sio ya kuaminika''

Kwenye ujumbe wa Twitter, balozi wa Iran katika IAEA, Gharib Abadi, alisema kuwa "kauli zozote za haraka zinapaswa kuepukwa", akiongeza kuwa: "mazungumzo yanaendelea kwa lengo la kukamilisha azimio la suala hilo ."


EmoticonEmoticon