Lil Wayne Arudiana Na Mpenzi Wake Baada Ya Trump Kushidwa Uchaguzi

 

Legend wa HipHop Duniani Lil Wayne Pamoja na mpenzi wake Denise Bidot , wanaonesha kurudisha Mapenzi yao Siku chache tu tangu Rais wa nchi hiyo Donald Trump kushindwa Kutetea kiti chake cha Urais.

Inaelezwa kwamba kitendo cha Lil Wayne kumuunga mkono Trump katika kipindi cha Kampeni, kilimkwaza sana Mwanadada Denise Bidot na kuamua kuvunja Penzi lake na Lil Wayne .

Kabla ya kuachana na Wayne, Denise aliandika kupitia Ukurasa wake wa Instagram "Muda Mwengine Mapenzi peke yake hayatoshi " , akimaanisha kua licha ya Mapenzi Lil Wayne aliyokua anampa, Lakini kitendo cha Kum-support Trump ilikua ni kama Usaliti .

Hata hivyo baada ya Trump Kushindwa Urais , wawili hao wameona wamalize tofauti zao .