Lil Wayne Huenda Akapigwa Miaka 10 Jela

 

Huenda rapa Dwayne Michael Carter  maarufu kama Lil Wayne (38) akafungwa miaka 10 gerezani akikutwa na hatia baada ya kushtakiwa kwa kosa la kumiliki silaha kinyume na sheria, kukutwa na madawa ya kulevya aina cocein na bangi.

Shtaka hilo ni la tukio lililotokea mwezi Desemba 2019 katika  Uwanja wa Ndege wa Miami Opa, Marekani, baada ya polisi kufanya upekuzi  ndani ya ndege ya msanii huyo.  Kesi ya rapa huyo  ilisomwa jana Jumanne Novemba 17 huko Miami nchini Marekani

Bosi huyo wa lebo ya Young Money, amekana mashtaka hayo na kesi yake itasomwa tena mwakani, 2021.

Hatua hii imekuja siku chache tangu rapa huyo alipotangaza kumuunga mkono Rais Donald Trump kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi huu.

Kitendo hicho kilimfanya mpenzi wake, Denise Bidot, kutangaza hadharani kuchukizwa na kitendo hicho na kuamua kuachana naye japokuwa baada ya  Joe Biden kushinda alisema amemsamehe na kurudisha mahaba tena.


EmoticonEmoticon