Maelfu Ya Wakaazi Walazimika Kuhama Nyumba Zao Kutokana Na Mafuriko Nigeria

Watu 158,000 wameripotiwa kuathirika kwa mafuriko yaliyosababishwa na mvua nyingi zilizonyesha katika mkoa wa Kebbi nchini Nigeria.

Msimamizi wa Shirika la Kitaifa la Maafa ya Dharura (NEMA) katika mkoa wa Kebbi na Sokoto, Alhaji Tukur Abubakar, alitoa maelezo na kusema kuwa watu 158,000 wameathirika kwa mafuriko yaliyosababishwa na mvua nyingi zilizonyesha katika maeneo 18 ya mkoa wa Kebbi mwezi Julai.

Abubakar aliongezea kusema kuwa maelfu ya watu wamelazimika kuacha nyumba zao zilizofunikwa na maji na kusababisha maisha kusimama kwa muda katika maeneo huku serikali ikijitahidi kuwasaidia.

Tangu mwezi Agosti hadi kufikia sasa, nchi ya Nigeria imekumbwa na maafa ya mafuriko yaliyosababisha watu wasiopungua 200 kupoteza maisha.


EmoticonEmoticon