Mahakama Yatupilia Mbali Kesi Ya Trump

 


Hali imezidi kuwa tete kwa Rais wa Marekani Donald Trump baada ya kesi ya udanganyifu wa kura pennsylvania ilioyofunguliwa na upande wake, kutupiliwa mbali na Jaji Matthew Brann ambayo ilitaka kubatilisha kura takriban Milioni 7 zilizopigwa kwa njia ya posta.

Amesema, upande wa Trump umeshindwa kuthibitisha kuna udanganyifu katika kura hizo. Uamuzi wa Jaji unaliruhusu Jimbo la kuthibitisha ushindi wa Joe Biden ambaye anaongoza kwa zaidi ya kura 80,000

Hili ni pigo jingine kwa Trump ambaye anajaribu kupindua matokeo ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika mapema mwezi huu, Rais huyo amekuwa akilalamikia udanganyifu licha ya kutokuwa na ushahidi wowote.


EmoticonEmoticon