Makamu Wa Kike Wa Kwanza Marekani Kamala Harris Atoa Neno La Shukrani Baada Ya Matokeo Ya Uchaguzi

 

Kwa upande wake, makamu wa rais mteule, Kamala Harris, ambaye anakuwa mwanamke wa kwanza na pia Mmarekani wa kwanza mwenye asili za Afrika na Asia Kusini kushikilia nafasi hiyo nchini Marekani, alitumia hotuba yake ya shukurani kuwashukuru maelsu ya wanawake wa Kiafrika waliothibitisha kwamba "wao ndio uti wa mgongo wa demokrasia" ya Marekani. 

Kamala, ambaye ni mtoto wa wahamiaji kutokea Jamaica na India, alisema kwamba amepata fursa hiyo ikiwa ni miaka 100 tangu Mabadiliko ya 19 ya Kativa ya Marekani na miaka 55 tangu kusainiwa kwa Sheria ya Upigaji Kura, ambayo iliruhusu idadi ya Wamarekani wenye haki ya kuchaguwa na kuchaguliwa.

Alisema Biden amevunja kikwazo kikubwa ambacho kimekuwapo kwenye siasa za Marekani kwa kumchaguwa yeye kuwa mwanamke wa kwanza na pia mwenye mizizi ya wahamiaji wa Kiafrika na Kiasia kuwa makamu wake. 


EmoticonEmoticon