Makombora Yarushwa Kuelekea Nchi Jirani Ya Eritrea

 

Makombora kutoka mkoa wa kaskazini wa Tigray nchini Ethiopia yameulenga mji mkuu wa Eritrea, Asmara saa kadhaa baada ya Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed kutangaza kumalizika kwa operesheni ya kijeshi katika eneo hilo. 

Abiy Ahmed alitangaza ushindi katika kampeni yake ya kijeshi dhidi ya chama tawala cha jimbo la Tigray (TPLF). 

Ubalozi wa Merekani katika mji mkuu wa Eritrea, Asmara uliripoti mapema Jumapili juu ya milipuko sita iliyotokea jijini humo Jumamosi usiku. 

Mashambulio hayo ya makombora ni kwa mara ya tatu yanayoulenga mji mkuu wa Eritrea, Asmara tangu kuanza operesheni ya kijeshi Novemba 4 dhidi ya utawala wa jimbo la Tgray katika nchi jirani ya Ethiopia, ingawa TPLF imedai kuhusika na shambulio la kwanza tu wiki mbili zilizopita. 

TPLF imehalalisha mashambulio hayo kwa kuilaumu serikali kuu ya Ethiopia kwa kupokea msaada wa jeshi la Eritrea katika operesheni yake kwenye jimo la Tigray, madai ambayo serikali ya Ethiopia imeyakanusha.


EmoticonEmoticon