Marekani Yaziwekea Vikwazo Kampuni Nne Za Iran

 

Marekani imetangaza vikwazo vya kiuchumi dhidi ya makampuni ya China na Urusi ambayo Washington inasema yamekuwa yakisaidia uendelezwaji wa programu ya nyuklia nchini Iran.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani, Mike Pompeo amesema kwenye taarifa yake kwamba makampuni manne yanayotuhumiwa kwa kuhamisha teknolojia ya hali ya juu pamoja na vifaa na kusaidia programu hiyo ya nyuklia ya Iran, yatalengwa na vizuizi vya misaada kutoka serikali ya Marekani na kuzuiwa kuingiza bidhaa zao nchini humo kwa miaka miwili.

Vikwazo hivyo vilivyowekwa kuanzia siku ya Jumatano vinayalenga makampuni mawili yaliyojikita nchini China, ya Chengdu Best New Materials na Zibo Elim Trade pamoja na kampuni ya Nilco Group and Joint Stock Company Elecon yenye makao yake Urusi. 

Marekani ilijiondoa kwenye mkataba wa nyuklia wa Iran mwaka 2018 na tangu hapo imekuwa ikiiwekea vikwazo Iran na kuathiri pakubwa uchumi wa taifa hilo la Kiislamu.


EmoticonEmoticon