Mashambulizi Yaendelea Ethiopia, Watu 32 Zaidi Waua

 

Watu waliokuwa wamejihami kwa bunduki wameua watu 32 na kuchoma moto zaidi ya nyumba 20 magharibi mwa Ethiopia.

Mauaji hayo yanaripotiwa kutekelezwa na kundi lenye silaha linalojiita OLF shane kutoka Wollega, eneo la Oromiya.

“tumezika watu 32 hii leo. Karibu watu 750 wameachwa bila makao,” amesema kiongozi wa eneo hilo Elias Umeta.

OLF Shane ni kundi ambalo liliundwa kutoka kwa kundi la Oromo Liberation Front (OLF), ambalo ni kundi la upinzani ambalo lilikuwa likiishi uhamishoni kwa mda wa miaka kadhaa lakini likakubaliwa kurudi Ethiopia baada ya waziri mkuu Abiy Ahmed kuingia madarakani mwaka 2018.

Matukio ya vurugu yamekuwa yakiripotiwa Ethiopia tangu kundi hilo lililiporudi nchini humo.

Kundi la OLF Shane linadai kupigania haki za watu kutoka jamii ya Oromos, ambayo ndio kubwa sana nchini Ethiopia.

Hakuna sababu maalum imetolewa kuhusiana na mauaji ya watu 32.

“wameuawa baada ya kuambiwa na watu hao waliokuwa na silaha kwamba walitaka kufanya nao mkutano,” amesema Elias.

Tume ya kutetea haki za kibiandamu inayoongozwa na serikali nchini Ethiopia, imesema kwamba shambulizi hilo lilikuwa limewalenga watu kutoka kabila la Amharic.

“Walichukuliwa kutoka nyumbani kwao na kupelekwa shuleni na kuuawa,” amesema Daniel Bekele, mkuu wa tume hiyo na kuongezea kwamba huenda idadi ya vifo ni ya juu zaidi inavyojulikana.

Ethipia imekuwa ikiripoti visa vya mauaji katika siku za hivi karibuni.


EmoticonEmoticon