Masoko Ya Hisa Yaimarika Kufuatia Uchaguzi Wenye Mchuano Mkali Nchini Marekan

 

Masoko ya hisa nchini Marekani yameimarika leo baada ya wawekezaji kupata matumaini kuwa matokeo ya uchaguzi yatazuia chama kimoja kuhodhi mabaraza mawili ya Bunge, hali itakayoondoa uwezekano kwa kufanyika mageuzi makubwa ya kisera kwa muda wa miaka 4 inayokuja. 

Ukuaji wa mitaji wa hadi asilimia 4.31 umeshuhudiwa kwenye sekta kadhaa ikiwemo teknolojia kufuatia imani ya wawekezaji kuwa thamani za hisa zitaendelea kupanda kwa sababu hakutakuwa na mabadiliko makubwa ya kisera mjini Washington. 

Ushindi usiotarajiwa wa seneta wa Republican Susan Collins wa jimbo la Maine umezima ndoto za chama cha Democratic za kuchukua udhibiti wa Baraza la Seneti ambalo ni muhimu katika kupitisha sera na mipango ya serikali. 

Hata hivyo wawekezaji wamesema bado wanatamani kuona mshindi wa kiti cha rais anapatikana na kufungua njia ya kufikiwa makubaliano ya mpango wa uokozi kwa uchumi wa Marekani ulioathiriwa na janga la virusi vya corona.


EmoticonEmoticon