Mfahamu Anayeshikilia Rekodi Ya Ngozi Ya Mwili Wake Kuvutika Sana Duniani

Gary Turner ni Muingereza anayeshikilia Rekodi ya Dunia ya Guinness ya kuivuta ngozi ya mwili wake. Oktoba 29, 1999 alivunja rekodi kwa kuvuta ngozi yake kwa urefu wa inchi 6.25.

Tangu avunje rekodi hiyo Garry Turner amekuwa akifanya maonyesho kwa kutumia ngozi yake na kujiingizia kipato.

Uwezo wa kuivuta ngozi umetokana na ugonjwa unaotambulika kama Ehlers-Danlos Syndromes (EDS) ambao kwake umejidhihirisha kwa kiasi kikubwa. 

EDS ni ugonjwa unaoleta madhara kwenye viungo ambao katika namna nyingine unaweza kumfanya mtu aweze kuzungushwa sehemu za mwili isivyo kawaida kama wanavyofanya baadhi ya wanasarakasi.


EmoticonEmoticon