Mitandao Ya Kijamii Kumkabithi Joe Biden Akaunti Za Serikali Baada Ya Kuapishwa

 

Twitter na Facebook wamesema watakabidhi account zote za Mitandao hiyo ya kijamii zilizo chini ya Ikulu ya Marekani kwa Rais mpya wa Marekani Joe Biden siku ya uapisho January 20 2021 huku wakisisitiza ni utaratibu wa kawaida kila Rais mpya anapoingia.

Account hizi hazihusu zile account binafsi za Donald Trump bali inahusu account zote za Ikulu na Taasisi zilizo chini yake kama account ya @ POTUS (President of the United States), ya Makamu wa Rais pamoja na ya First Lady.


Twitter imesema "Mwaka 2017 tulishirikiana na Uongozi wa Obama na tukachukua aacount hizo na kuukabidhi Uongozi wa Donald Trump uliokua ukiingia madarakani, tutafanya vivyohivyo kwa Rais mpya Joe Bidden siku ya uapisho January 20 2021"

Imeripotiwa kuwa upokezanaji wa account hizo ikiwemo Twitter ya POTUS hautakiwi kuwa wa wazi kati ya hizo pande mbili (Rais anaeachia Ikulu na ambae anaingia Ikulu) ndio maana Twitter inaingia kati na kufanya makabidhiano hayo kwa Uongozi wa Rais mpya bila uongozi unaoondoka kufahamu taarifa nyeti za account hiyo ikiwemo password mpya n.k


EmoticonEmoticon