Mji Mkuu Wa Tigray Unakabiliwa Na Mashambulio Makali

 

Mji mkuu wa jimbo la Tigray kaskazini mwa Ethiopia unakabiliwa na mashambulio makali ya kutoka kwa vikosi vya serikali, wafanyakazi wa misaada na maafisa wa eneo hilo wanasema.

Eneo la kati kati ya mji wa Mekelle linashambuliwa kwa "makombora," chama tawala katika jimbo la Tigray kinasema.

Kiongozi wa TPLF Debretsion Gebremichael ameambia shirika la habari Reuters kupitia ujumbe wa simu kwama mji wa Mekelle unakabiliwa na "mashambulio makali ya makombora", na kuongeza kuwa vikosi vya serili vimeanza oparesheni ya kuteka mji huo.

Taarifa tofauti kutoka kwa TPLF, iliyoripotiwa na shirika la habari la AFP, inatoa wito kwa "jamii ya kimataifa kulaani mashambulio hayo ya angani kwa kutumia ndege za kivita kutekeleza mauaji".

Pia imelaumu serikali ya Eritrea kwa kuhusika na mashambulio katika mji wa Mekelle.


EmoticonEmoticon