Mke Wa Donald Trump Yupo Mbioni Kuitaka Talaka Yake

 

Donald Trump ameshindwa Urais wa Marekani lakini pia hivi karibuni atamkosa mkewe, Melania Trump.

Mtandao wa Daily Mail umeripoti kwamba msaidizi wa zamani wa Melania Trump, Ms Walkoff amesema first lady huyo yupo mbioni kukamilisha faili la talaka na kuachana na Trump ambaye wamedumu kwenye ndoa kwa miaka 15 na kupata mtoto mmoja, Barron Trump.

Ms Walkoff anasema Melania alitokwa na machozi kipindi mumewe ameshinda Urais mwaka 2016, kwani inaelezwa kwamba hakutarajia kama angeshinda. Kwa inavyoonekana ni kama Melania hakutaka kuwa First Lady kwani ilimchukua miezi mitano kutoka New York na kuhamia Washington ilipo White House.

Aliendelea kutufunulia yaliyo nyuma ya pazia kwamba Trump na Melania walikuwa wakilala vyumba tofauti ndani ya ikulu ya Marekani. Hiyo inakaziwa na zile tabia tulizokuwa tukiziona mbele ya hadhira kwa muda mwingine Melania kukataa kushikwa mkono na mumewe.

Kinachosubiriwa ni Trump akabidhi madaraka kwa Rais ajaye ndipo akamilishe talaka kwani kwa sasa haiwezekani kwa sababu mumewe bado ni Rais na anatakiwa kuwa na mke.