Mkutano Wa G20 Waanza Chini Ya Kiwingu Cha Janga La COVID-19

 

Mkutano wa kilele wa kundi la mataifa yaliyoendelea na yale yanayoinukia kiuchumi G20 unaanza leo Jumamosi chini ya mwenyeji Saudi Arabia, ukigubikwa hata hivyo na kiwingu cha janga la virusi vya corona. 

Shughuli za mkutano huo wa kilele ambao kwa kawaida huwakutanisha ana kwa ana viongozi wa madola yenye nguvu zimepunguzwa na badala yake kutakuwa na majadiliano mafupi kupitia njia ya video kuhusu masuala tete yanayoukabili ulimwengu hususan athari za janga la virusi vya corona.

Kadhalika kutakuwa na mjadala kuhusu mabadiliko ya tabia nchi na kuongezeka kwa ukosefu wa usawa duniani

Saudi Arabia ambayo ndiyo mwenyeji wa mkutano huo wa siku mbili imekuwa nchi ya kwanza ya kiarabu kuandaa mkutano wa G20.

Rais Donald Trump wa Marekani atakuwa sehemu ya viongozi watakoshiriki mkutano huo  wa kilele wa kundi la G20.

Taarifa hizo zimethibitishwa na afisa wa ngazi ya juu wa serikali ya Marekani ambaye amesema Trump atakuwa sehemu ya viongozi wa ulimwengu watakaoshiriki mkutano huo unaofanyika kwa njia ya video kutokana na janga la virusi vya corona.


EmoticonEmoticon