Mkutano Wa Majadiliano Wa Libya Washindwa Kufikia Makubaliano Ya Serikali

 

Mazungumzo yaliyosimamiwa na Umoja wa Mataifa yenye lengo la kuteuwa serikali ya mpito nchini Libya ili kukomesha mzozo wa muongo mzima sasa, yamemalizika bila ya kuutaja uongozi wa serikali hiyo. 

Kaimu Mjumbe wa Umoja wa Mataifa kwa Libya, Stephanie Williams, amewaambia waandishi wa habari kwamba wameamua kuendelea na mkutano mwengine ndani ya wiki moja kuhusu jinsi ya kuupata uongozi huo.

Mkutano huo wa wiki moja, ambao ulikuwa hatua ya hivi karibuni kabisa kusaka suluhisho la kisiasa kwa mzozo wa Libya, uliwahusisha wajumbe 75 waliochaguliwa na Umoja wa Mataifa kuwakilisha makundi muhimu ya Libya.

Wajumbe hao walipewa jukumu la kubuni mpango wa kuipeleka Libya kwenye uchaguzi, kuamua juu ya mamlaka utakayokuwa nayo uongozi wa serikali ya mpito na kuwataja wajumbe wa serikali hiyo.


EmoticonEmoticon