Mtoto Azaliwa Na Kinga Ya Corona Huko Singapore

 

Wakati dunia bado ikiendelea kuhangaika kutafuta Chanjo / Kinga ya Mwili, Mama mmoja wa huko nchini Singapore amejifungua mtoto ambae ana Kingamwili (antibodies) dhidi ya Virusi vya Corona .

Celine Ng-Chang Mwenye umri wa miaka 31, amejifungua mtoto huyo Mwezi huu baada ya kufanikiwa kupona Virusi vya Covid-19 akiwa mjamzito .

"Madaktari wameniambia kwamba ntakua nimemuhamishia Mtoto wangu kinga za Covid-19 nikiwa mjamzito " - alisema Mama huyo .

Kwa mujibu wa wataalamu wa afya, mtu mwenye Kingamwili za Covid-19 anaweza kutoambukizwa Virusi hivyo, Japo bado haijafahamika ni kwa kiwango gani .


EmoticonEmoticon