Muigizaji Wa Filamu Ya James Bond Afariki Dunia

Sir Sean Connery, muigizajiwa sinema ya James Bond amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 90, familia yake imethibitisha.

Muigizaji huyo wa Uskochi alifahamika sana kwa kuwa mhusika wa katika sinema ya James Bond, na alikuwa wa kwanza kuleta sinema hiyo katika ukumbi wa sinema..

Sir Sean alifariki akiwa usingizini, akiwa Bahamas ambako amekuwa "akiugua kwa muda", mwanawe wa kiume alisema.

Kazi yake ya uigizaji wa miongo mitano ilimwezesha kushinda tuzo ya Oscar mwaka 1988 kutokana na jukumu lake katika 'The Untouchable'.

Filamu zingine alizoigiza Sir Sean ni pamoja na The Hunt for Red October, Highlander, Indiana Jones na the Last Crusade and The Rock.

Jason Connery alisema baba yake "alikuwa na sehemu kubwa ya familia yake Bahamas ambayo ilikuwa naye" alipofariki usiku mjini Nassau.

Alisema: "Sote tunajaribu kukubaliana na msiba huu mkubwa kwani limetokea sasa, ingawa baba yangu amekuwa mgonjwa kwa muda.

"Ni siku ya huzuni kwa watu wate waliomfahamu baba yetu mpendwa na watu wote waliovutiiwa na uigizaji wake kote duniani ." 


EmoticonEmoticon