NATO, EU Wamwalika Biden Kujenga Upya Uhusiano Na Marekani

 

Rais mteule wa Marekani Joe Biden amezungumza na viongozi wa taasisi ya Umoja wa Ulaya, na Jumuia ya kujihami ya NATO kama sehemu ya juhudi zake za kuurekebisha uhusiano uliovunjika ambao unavuka Bahari ya Atlantiki. 

Taarifa kutoka ofisi ya Biden imesema rais huyo mteule amesisitiza umuhimu wa kuufufua uhusiano wa Marekani na Umoja wa Ulaya, baada ya kumpigia simu rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya, Ursula Von der Leyen. 

Tofauti na matamshi ya Donald Trump ya kuuita umoja huo adui na kuushutumu kuinyima Marekani biashara, Joe Biden ameelezea matumaini yake kwamba pande hizo mbili zitashirikiana katika changamoto zinazowakabili.

Von der Leyen kwa upande wake ameonekana kufurahishwa na mazungumzo yake na Biden baada ya kuandika hivi katika ukurasa wake wa Twitter kwamba "Nafurahi kuzungumza na rais Mteule Joe Biden, huu ni mwanzo mpya wa ushirikiano baina ya Umoja wa Ulaya na Marekani. 

Kufanya kazi pamoja kunaweza kuijenga ajenda ya dunia kuhusu ushirikiano wa kimataifa, mshikamano na maadili ya pamoja.


EmoticonEmoticon