Pompeo Azuru Makaazi Ya Wayahudi Katika Ukingo wa Magharibi

 

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani Mike Pompeo amekuwa mwanadiplomasia mkuu wa kwanza wa Marekani kuitembelea Milima ya Golan inayokaliwa na Israel baada ya kuzuru makaazi ya Wayahudi katika Ukingo wa Magharibi kitendo kilichowakasirisha Wapalestina. 

Ziara hiyo ya Pompeo katika maeneo hayo tete ni ishara muhimu kutoka kwa serikali inayoondoka ya Marekani. 

Pompeo amemwambia Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kuwa Marekani italichukulia vuguvugu la kimataifa ya Kususia, Kuondoa Uwekezaji na kushinikiza Vikwazo kuwa la kueneza chuki dhidi ya Wayahudi. 

Pompeo amesema Marekani itaondoa msaada wa serikali kwa makundi yanayoshirikiana na vuguvugu hilo linaloongozwa na Palestina. 

Netanyahu kwa upande wake alimshukuru Pompeo na Rais anayeondoka Donald Trump kwa uungaji mkono wao kwa miaka minne iliyopita. 

Ziara hiyo ya Pompeo katika makaazi ya Wayahudi imelaaniwa na viongozi wa Kipalestina. 

Msemaji wa rais wa Wapalestina Mahmud Abbas amesema uamuzi wa Pompeo unakiuka wazi sheria ya kimataifa.


EmoticonEmoticon