Rais wa
zamani wa Ufaransa Nicolas Sarkozy atafika mahakamani Jumatatu ambapo
anatuhumiwa kujaribu kutoa hongo kwa jaji na kupelekea ushawishi,ikiwa ni moja
ya uchunguzi kadhaa wa jinai ambao unatishia kuweka aibu kubwa katika utumishi
wake wa muda mrefu wa kisiasa.
Waendesha mashtaka wanadai
Sarkozy alijitolea kumpatia kazi ya fedha nyingi Jaji Gilbert Azibert huko
Monaco kwa malipo ya habari ya siri juu ya uchunguzi wa madai kwamba Sarkozy
alikuwa amekubali kupokea malipo haramu kutoka kwa mrithi wa L'Oreal Liliane
Bettencourt kwenye kampeni yake ya urais ya mwaka 2007.
Sarkozy, ambaye aliongoza
Ufaransa kutoka mwaka 2007 hadi 2012 na amebaki na ushawishi mkubwa kati ya
wahafidhina, amekanusha makosa yoyote katika uchunguzi wote dhidi yake na
kupambana vikali ili kesi hizo zifutwe.
Wachunguzi kutoka mwaka
2013 walikuwa wakisikiliza mazungumzo kati ya Sarkozy na wakili wake Thierry
Herzog walipokuwa wakichunguza madai ya ufadhili wa Libya katika kampeni ya
Sarkozy ya mwaka 2007.
Wakati wakichunguza waligundua kwamba Sarkozy na wakili wake walikuwa wakiwasiliana kwa kutumia simu za mkononi zilizosajiliwa kwa majina ya uwongo. Simu ya Sarkozy ilisajiliwa kwa jina la Paul Bismuth.
EmoticonEmoticon