Serikali Scotland Yaanza Kutoa Taulo za Kike Bure

 

SCOTLAND limekuwa taifa la kwanza duniani kufanya bidhaa za sodo/pedi kugawiwa bure kwa kila mtu. Wabunge walipitisha mswada huo bila kutoa taarifa siku ya Jumanne.

Na sasa mamlaka imetoa idhini kisheria kuhakikisha kuwa bidhaa hizo zinatolewa bure kwa yeyote anayehitaji. Mswada huo uliletwa na Waziri wa Ajira, Bi. Monica Lennon, akilenga kuendesha kampeni ya kukomesha umaskini wa kununua bidhaa hizo tangu mwaka 2016.

Alisema kuwa ni suala linalowezekana kufanyika na sheria tu ndiyo inaweza kutoa mwongozo wa kila kitu na sasa ni muhimu zaidi kutokana na janga la corona.

“Siku za hedhi haziachi kutoka wakati wa janga lolote na kazi kubwa inapaswa kufanywa kuhakikisha pedi au sodo hizo zinatolewa bure,” aliongeza.

Umasikini wa sodo ukoje? Umasikini wa sodo ni pale watu wenye kipato cha chini wanaposhindwa kununua pedi. Boksi moja la pedi zinazoweza kutumika siku tano zinagharamu ya paundi 8 na baadhi ya wanawake hawawezi kumudu gharama hiyo.


EmoticonEmoticon