Tathmini Zinaonyesha Joe Biden Anayo Nafasi Kubwa Ya Kumshinda Trump Katika Uchaguzi

 

Mgombea urais kwa kupitia chama cha Democratic nchini Marekani, Joe Biden, anaongoza kwa point 10 dhidi ya rais wa sasa wa nchi hiyo, Donald Trump.

Hojaji iliyofanywa na Shirika la Habari la NBC na gazeti la Wall Street imeonyesha kuwa, idadi ya wapiga kura walioandikishwa kumuunga mkono Joe Biden imefikia asilimia 52 dhidi ya asilimia 42 ya wanaomuunga mkono rais Trump.

Hojaji hii ya mwisho imefanyika kuanzia Oktoba 29 hadi 31, pia imeonyesha kuwa Joe Biden ana nafasi kubwa zaidi kwa wapiga kura Wamarekani wenye asili ya Afrika, vijana, wazee na wanawake.


EmoticonEmoticon