Trump Adai Kushinda Asipoibiwa Kura Na Democratic

Rais Donald Trump wa Marekani ametoa madai ya kufanyiwa wizi katika uchaguzi mkuu wa taifa hilo pasipo na kuwa na ushaihidi wowote. 

Rais huyo amesema mahasimu wake chama cha Democratic, wanafanya jaribio la wizi katika uchaguzi huo ambao alidai yeye anaweza kushinda kwa urahisi kabisa dhidi ya Joe Biden. 

Akizungumza katika Ikulu ya Marekani na kunukuliwa na vyombo kadhaa vya habari alisika akisema "Kama ukihesabu kura halali, nitashinda kwa wepesi.

Lakini kama utahesabu kura zisizo halali, wanaweza kutuibia uchaguzi huu." Hadi wakati huu timu ya kiongozi huyo imeanzisha kiasi kwa kiwango kikubwa cha madai katika lengo la kukabiliana kile alichokiita "ufisadi" wa chama cha Democrat. 

Hata hivyo maafisa katika baadhi ya majimbo ya uchaguzi bado hayajatoa uamuzi kuhusu malalamiko hayo.


EmoticonEmoticon