Trump Afungua Mashtaka Akilalamikia Mchakato Ya Kuhesabu Kura

Donald Trump na Joe Biden wote kwa pamoja wanadai kuongoza katika uchaguzi mkuu wa Marekani wakati huu matokeo ya mwisho yakiwa mbioni kutolewa na pande zote mbili kudai kuchukua hatua za kisheria.

Kampeni ya Trump imekosoa mchakato wa kuhesabu kura katika majimbo muhimu ya Wisconsin, Georgia, Pennsylvania na Michigan.

BBC inatabiri kuwa Bwana Biden alishinda Michigan. Vyombo vya habari vya Marekani vinatabiri kuwa amelinasa jimbo la Wisconsin. Hakuna matokeo yaliyotolewa katika jimbo la Pennsylvania.

Kuongza katika majimbo yote matatu muhimu kutampa ushindi Biden. Bwana Biden aliacha kutangaza kuwa ameshinda, lakini akasema alikuwa na uhakika alikuwa njiani kumshinda Donald Trump.

Kwa ujumla waliojitokeza kwenye uchaguzi wa siku ya Jumanne inaelezwa kuwa idadi kubwa kuwahi kutokea katika kipindi cha miaka 120 ambayo ni 66.9% imeelezwa na mamlaka za uchaguzi.


EmoticonEmoticon