Trump Akiri Biden Kushinda Uchaguzi Marekani

Donald Trump alisisitiza kuwa hakubaliani na matokeo ya uchaguzi wa Marekani, lakini ameonekana kukubali matokeo kwa mara ya kwanza kuwa mpinzani wake wa Democrat Joe Biden ameshinda.

"Ameshinda uchaguzi kwa kuwa mchakato wa uchaguzi ulikuwa wa wizi," ameandika kwenye kurasa yake ya Twitter lakini baada ya dakika chache alisema hamaanishi kuwa alishindwa uchaguzi wa Novemba 3.

Bwana Trump alirudia tena madai yake ya kuibiwa katika uchaguzi. Alifugua kesi kuhusu madai yake lakini hakutoa ushaidi wowote wa madai yake ya kuibiwa. Mashtaka yake yote yamepuuziwa.

Ijumaa, maafisa wa uchaguzi walisema uchaguzi ulifanyika katika usalama zaidi katika historia ya Marekani na hakuna ushaidi kuwa kura zilipotea au kuibiwa au kuwa na tatizo lolote la kufanya uchaguzi kutiliwa shaka.

Pamoja na ufafanuzi huo , Trump hakukubali kuwa Biden alishinda uchaguzi mpaka sasa. 


EmoticonEmoticon