Trump Akubali Kuanza Kumkabidhi Madaraka Joe Biden

 

Donald Trump amekubali kuanza kwa mchakato rasmi wa kumkabidhi madaraka Rais mteule Joe Biden.

Rais amelitaka shirika linaloshughulikia mabadilishano hayo "lifanye kile kinachostahili kufanywa", hata wakati anaahidi kuendelea kupinga matokeo.

Ofisi ya utawala wa huduma za serikali imesema inamtambua Bwana Biden kama "mshindi".

Trump aliandika ujumbe kwenye mtandao wa Twitter wakati ofisi ya utawala wa huduma za serikali ambayo ndiyo yenye jukumu rasmi la kuanza mchakato wa mabadilishano ya madaraka inaarifu timu ya Biden kwamba itaanza mchakato huo.

Afisa wa ofisi hiyo Emily Murphy alisema dola milioni 6.3 sawa na (£4.7m) amezitenga kwa ajili ya rais mteule.

Wakati anaahidi kuendelea na "vita hivyo muhimu", rais alisema: "Haidhuru, kwa maslahi ya nchi yetu, Napendekeza Emily na timu yake kufaya kile kinachostahili kwa kuzingatia itifaki za awali na pia nimearifu timu yangu kufanya vivyo hivyo."

Bi. Murphy, aliyeteuliwa na Trump alitaja "matukio ya hivi karibuni ya kisheria yanayopinga matokeo ya uchaguzi" katika uamuzi wake wa kutuma burua hiyo.

Amesema hajapokea shinikizo lolote kutoka Ikulu ya Marekani kwa muda ambao ametoa uamuzi wake.

"Kuwa wazi, sikupokea maagizo yoyote ya kuchelewa kufanya uamuzi wangu," Barua ya Murphy kwa Biden imesema.

"Lakini nilipokea vitisho kwa njia ya mtandao na barua pepe vilivyoelekezwa kwa usalama wangu, familia yangu, wafanyakazi wangu na hata wanyama wangu wa nyumbani kushinikiza kufanya uamuzi huu mapema.

"Hata wakati nakabiliwa na vitisho elfu kadhaa nimeendeelea kuhakikisha sheria inafuatwa."

Murphy alikosolewa na pande zote za kisiasa kwa kushindwa kuanza mchakato wa mabadilishano ya madaraka mapema ambao kawaida huwa ni kati ya kipindi cha uchaguzi na hafla ya kuapishwa.

Bi. Murphy alishindwa kufikia siku ya ukomo ya Jumatatu ya kuanza shughuli hiyo iliyokuwa imetengwa na wabunge wa chama cha Democratic katika bunge la wawakilishi kuwaarifu wabunge hao kuhusu kuchelewa kuanza kwa shughuli hiyo.


EmoticonEmoticon