Trump Ametangaza Uamuzi Atakaochukua Endapo Atashindwa Uchaguzi (VIDEO)

 

Huku kukiwa na kura nyingi tu ambazo bado hazijahesabiwa, Donald Trump amedai kuwa ameshinda.

“Ukweli ni kwamba tumeshinda,” amedai hivyo akizungumza kwa sauti ya upole. Bila ushahidi wowote – Trump amedai kuwa uchaguzi umekubwa na ” udanganyifu”.

“Hii ni aibu kwa nchi yetu,” Trump amesema, na kuongeza kwamba anapanga kwenda mahakama ya juu zaidi kupinga matokeo ya uchaguzi.

Mamilioni ya kura katika uchaguzi wa Marekani mwaka 2020 bado hazijahesabiwa na rais hana haki yoyote ya kujitangaza mshindi.


EmoticonEmoticon