Trump Aonyesha Ishara Za Kuwa Tayari Kuondoka Madarakani

Rais Donald Trump wa Marekani amesema ataondoka Ikulu ikiwa Joe Biden atathibitishwa rasmi kuwa rais anayefuata wa Marekani kwa kura za wajumbe. 

Alipoulizwa Alhamisi ikiwa atakubali kuondoka Ikulu ya Marekani kama alishindwa katika kura za wajumbe, alisema: "Bila shaka nitaondoka, nitaondoka na munajua hivyo."

Hata hivyo, aliendelea kusema kuwa "ikiwa watamchagua [Joe Biden], wamefanya makosa", na kuonesha kana kwamba huenda asikukubali matokeo.

"Itakuwa jambo gumu sana kukubali kushindwa kwasababu tunajua kulikuwa na wizi mkubwa wa kura," amesema, madai ambayo amekuwa akiyataja kila wakati bila kutoa ushahidi. Aidha, hakusema ikiwa atahudhuria sherehe ya kuapishwa kwa Biden. 


EmoticonEmoticon