Trump Apelekea Lil Wayne Kuachwa Na Mpenzi Wake Denise Bidot

 

Rapa Lil Wayne arudi tena kuwa Single, ameripotiwa kuachwa na mpenzi wake wa hivi karibuni Denise Bidot kwa kile kilichotajwa kuwa ni kitendo chake cha kuamua kumuunga mkono Rais Donald Trump.

Tovuti za TMZ na Love B. Scott zimeripoti kwamba Denise alithibitisha hilo kupitia ukurasa wake wa Instagram ambao tayari ameufuta kwa sasa (deactivate), lakini pia watu wa karibu na mrembo huyo wamesema, alivunjika moyo baada ya kuona Wizzy anamuunga mkono Rais Trump.

"Ameachana na Lil Wayne. Sio tu kwa sababu za kumuunga mkono Trump, lakini hiyo ndio sababu kubwa." Wamesema marafiki zake Denise Bidot.


EmoticonEmoticon