Trump Awasilisha Maombi Ya Kura Kuhesabiwa Upya

 

Rais wa Marekani Donald Trump amewasilisha maombi ya kutaka kura katika jimbo la Wisconsin, kurudiwa kuhesabiwa.

Trump anataka kura kuhesabiwa upya katika majimbo mawili makubwa ambayo yana idadi kubwa ya wafuasi wa chama cha Democratic, akidai kwamba wizi wa kura ulifanyika katika majimbo hayo.

Hakuna Ushahidi wowote umetolewa kudhibitisha madai yake. Amelipa dola milioni 3 zinazohitajika ili kura hizo kuhesabiwa upya.

Shughuli hiyo inatarajiwa kuanza leo alhamisi na ni lazima ikamilike kabla ya Desemba tarehe moja.


EmoticonEmoticon