Uingereza Yasema Mazungumzo Ya Kibiashara Na EU Yako Katika Wiki Yake Ya Mwisho

 

Waziri wa mambo ya kigeni wa Uingereza Dominic Raab amesema imesalia wiki moja kwa nchi yake na Umoja wa Ulaya kufikia makubaliano ya kibiashara katika mazungumzo ya Brexit kabla Ungereza kujiondoa kutoka kwenye umoja huo mwishoni mwa mwaka huu.

Hata hivyo haki za uvuvi bado ni kizingiti kikubwa katika mazungumzo hayo. Umoja wa Ulaya unataka wavuvi wake waendelee kuwa na haki ya kuvua kwenye bahari ya Uingereza lakini hatua hiyo inapingwa vikali na Uingereza ikitaka udhibiti wa bahari yake bila ya kuwekewa masharti. 

Mazungumzo kati ya pande hizo mbili yanaendelea mjini London. Uingereza ilijiondoa katika Umoja wa Ulaya mapema mwaka huu lakini ikabakia kuwa sehemu ya biashara umoja huo ulio na wanachama 27 wakati wa miezi 11 ya mpito huku pande zote mbili zikijaribu kufikia makubaliano ya biashara huru yanayotarajiwa kuanza rasmi Januari mosi mwakani.


EmoticonEmoticon