Ujerumani Yaanza Kutekeleza Vizuizi Kudhibiti Virusi Vya Corona

 

Ujerumani imeanza kuzifunga baadhi ya shughuli za umma nchini kote kwa muda wa mwezi mmoja kwa lengo la kudhibiti kasi ya maambukizi ya virusi vya corona ambapo watu nusu milioni wameambukizwa. 

Hata hivyo, taasisi ya kudhibiti magonjwa ya kuambukiza ya Ujerumani, Robert Koch imeripoti kupungua kwa maambukizi mapya yaliyofikia watu alfu 12 katika muda mfupi uliopita. 

Lakini kwa upande mwingine maambukizi hayo yalikuwa yanaongozeka sana katika wiki za karibuni. Hatua zilizotangazwa na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel safari hii siyo kali kulinganisha na za hapo awali. 

Shule, maduka na makanisa yataendelea na shughuli kama kawaida na maandamano hayatapigwa marufuku. Hata hivyo mikahawa, sehemu za burudani ya vileo, sehemu za kuogelea na za michezo zitafungwa. 

Mikutano ya hadharani itakayoruhusiwa ni ile ya watu kutoka kaya mbili tu. Viongozi wa serikali kuu na wa majimbo watakutana baada ya siku 10 kufanya tathmini iwapo hatua hizo zitapaswa kuimarishwa zaidi au kulegezwa, kutegemea na idadi ya maambukizi.


EmoticonEmoticon