Ulinzi Na Usalama Kwa Joe Biden Waongezwa Baada Ya Kuonekana Kunusa Ushindi

 

Usalama umeimarishwa kwa Joe Biden kuanzia Ijumaa wakati inatarajiwa kuwa huenda akatangazwa kuwa mshindi, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na gazeti la Washington.

Bwana Biden ataongezewa idadi ya maafisa wa usalama baada ya timu yake ya kampeni kuiambia idara husika kwamba anaweza akatoa hotuba muhimu Ijumaa, gazeti hilo limeandika kwa kunukuu watu wenye ufahamu wa mipango hiyo.

Bwana Biden na timu yake ya kampeni wamekuwa katika kituo cha Wilmington, Delaware.


EmoticonEmoticon