Umoja Wa Mataifa Waonya Kuhusu Mzozo Wa Kiutu Ethiopia

 

Umoja wa Mataifa umesema mzozo kamili wa kibinaadamu unajitokeza kaskazini mwa Ethiopia, ambako maelfu ya watu kila siku wanalikimbia jimbo lenye machafuko la Tigray. 

Wakati shinikizo la kimataifa likiongezeka kuhusu kampeni yake dhidi ya viongozi waasi wa Tigray, Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed ametangaza kuwa operesheni zinaingia katika awamu ya mwisho. 

Serikali ya Abiy imethibitisha kufanyika mashambulizi mapya ya anga karibu na mji mkuu wa Tigray, Mekele. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia wakimbizi, UNHCR limesema Waethiopia 27,000 wamekimbilia mashariki mwa Sudan. 

Msemaji wa UNHCR, Babar Baloch amesema wimbi hilo la wakimbizi halijawahi kushuhudiwa Sudan katika miongo miwili iliyopita. Abiy mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel kwa mwaka uliopita, Novemba 4 alitangaza operesheni ya kijeshi kujibu mashambulizi yaliyofanywa na vikosi vya chama tawala cha Ukombozi wa Watu wa Tigray, TPLF, dhidi ya kambi za jeshi la Ethiopia.


EmoticonEmoticon