Uturuki Yawahukumu Maisha Jela Waliofanya Jaribio La Mapinduzi

 

Mahakama moja ya Uturuki imewahukumu kifungo cha maisha watu wapatao 500 wakiwemo makamanda wa jeshi na marubani, wanaotuhumiwa kuongoza jaribio la mapinduzi mwaka 2016 kutoka kituo cha jeshi la anga karibu na mji mkuu, Ankara.

Zaidi ya watu 250 waliuawa Julai 15, 2016 baada ya wanajeshi waasi walipochukua udhibiti wa ndege za kivita na vifaa vyengine vya vita katika jaribio la kutaka kuipindua serikali ya Rais Tayyip Erdogan.

Kesi hiyo ni miongoni mwa kesi kubwa nchini humo zinazolenga watu waliohusika na jaribio hilo la mapinduzi.Serikali inadai liliongozwa na wafuasi wa mhubiri wa Kiislamu Fethullah Gulen mwenye makao yake nchini Marekani.


EmoticonEmoticon