Vifo vya Covid 19 Vyapindukia 1, 305, 039 Duniani kote

 

Kiasi ya watu 1, 305, 039 wamefariki kutokana na virusi vya corona tangu vilivyoripotiwa kwa mara ya kwanza nchini China mwishoni mwa mwaka uliopita.

Kwa mujibu wa takwimu za shirika la habari la AFP, watu wasiopungua 53, 483, 640 wameambukizwa virusi hivyo kote duniani. 

Kati ya idadi hiyo, watu milioni 34, 324, 500 wamepona.Takwimu hizo ambazo zimekusanywa kwa kujumuisha taarifa zinazotolewa na serikali mbalimbali duniani na pia kutoka shirika la afya duniani WHO, huenda zinaonyesha sehemu ndogo tu ya idadi kamili ya watu walioambukiwa virusi hivyo.

Nchi iliyoathirika zaidi na janga la Covid-19 ni Marekani iliyorekodi vifo 244,364 ikifuatiwa na Brazil yenye vifo 164, 737 na India ni ya tatu kwa kurekodi vifo 129,188 vinavyotokana na ugonjwa huo wa mapafu.


EmoticonEmoticon