Viongozi Wa Uarabuni Wakabiliwa Na Changamoto Mpya Baada Ya Ushindi Wa Joe Biden

 

Itabidi unisamehe ikiwa ninaonekana kuvurugika kidogo," alisema balozi wa Saudi Arabia nchini Uingereza huku macho yake yakiangaza kwa simu ya mkononi. "Nafuatilia matokeo ya uchaguzi katika jimbo la Wisconsin."

Hiyo ilikuwa siku nane zilizopita, kabla haijabainika ni nani atakayeingia Ikulu White House mwezi Januari mwakani.

Wakati Joe Biden alipotangazwa mshindi, uongozi wa Saudia mjini Riyadh ulichukuwa muda kujibu ikilinganishwa na jinsi ulivyofanya wakati Donald Trump alipochaguliwa.

Hii haishangazi: walikuwa wamepoteza rafiki muhimu. Ushindi wa Bwana Biden sasa unaweza kuwa na athari kwa Saudi Arabia na mataifa mengine ya Ghuba.

Ushirikiano wa kimkakati wa Marekani katika eneo hilo ulianza mnamo mwaka 1945 na unatarajiwa kudumu, lakini mabadadiliko ya utawala unaokuja huenda yasipokelewe na wote katika miji mikuu ya Ghuba


EmoticonEmoticon