Wachezaji Wa Barcelona Akiwemo Messi Wakubaki Kukatwa Mishahara

 

Mastaa wa Barcelona wakiongozwa na Lionel Messi wamekubaliana na klabu hiyo kukubali kupunguziwa mishahara yao ambayo inathamani kiasi cha pauni 110m kwa msimu huu.

Barcelona imeamua kufanya hivyo kutokana na hali ngumu ya kiuchumi ambayo inaikabili klabu hiyo kwa sasa kutokana na janga la virusi vya corona. 

Imeelezwa kuwa baada ya majadiliano ndani ya klabu hiyo wamefikia muafaka kwa wachezaji hapo kupunguziwa mshahara kwa msimu huu wa 2020/21 wakiongozwa na Messi.

Taarifa ya klabu ilieleza: “Haya makubaliano ni kama ya muda ambayo baada ya makubaliano yameonekana kuwaathiri wachezaji pamoja na makocha.

“Hii ni kutokana na hali halisi ya uchumi wa sasa wa ndani ya klabu pande zote mbili zimekubaliana kwenye hili kutokana na hali ya
sasa.” Barcelona imekumbana na hali ya COVID-19 ambayo imetikisa dunia hivyo, wachezaji wamekubalia kupunguziwa mishahara
kwa asilimia 70.

Klabu hiyo ilitoa taarifa Oktoba mwaka kuwa imepoteza kiasi cha pauni 88m na hii ilikuwa ni kutokana na janga la corona.


EmoticonEmoticon