Wajumbe katika kongamano la wafadhili wa kimataifa juu ya Afghanistan, wameahidi kutoa kiasi cha dola bilioni 12, ndani ya miaka minne ijayo ili kuisadia nchi hiyo iliyokumbwa na vita.
Katika
mkutano huo uliofanyika mjini Geneva kwa njia ya vidio, nchi wafadhili
zimekubali kuendelea kuisadia nchi hiyo ambayo imegubikwa na machafuko baina ya
wapiganaji wa Taliban na serikali, ufisadi mkubwa na kuondolewa kwa wanajeshi
wa Marekani.
Waziri wa ushirikiano wa
maendeleo na biashara ya kigeni wa Finland Ville Skinarri, alisema nchi
wafadhili wameahidi kutoa dola bilioni 3 mwaka ujao, huku kiasi hicho
kikitarajiwa kuendelea kutolewa kila mwaka hadi kufikia 2024 na hivyo kufanya
jumla ya ufadhili kufikia dola bilioni 12.
Nchi nyingi zimetoa
masharti kwa Afghanistan juu ya kuheshimu mchakato wa amani na kutaka uongozi
bora ili kuboresha demokrasia na kupambana na ufisadi. Jumuiya ya kimataifa
ilitaka pia "usitishwaji wa kudumu wa mapigano", wakati watu
wasiopungua 14 wakiuawa katikati mwa Afghanistan pale milipuko miwili ilipotokea
katika mji wa kihistoria wa Bamiyan.Afghanistan yatangaza timu ya mazungumzo na
Taliban
Waziri wa mambo ya kigeni
wa Afghanistan Mohammad Haneef Atmar amesifu kiasi kilichopatikana, akiongeza
kuwa " ni muhimu zaidi kwasababu mchango huo umekuja wakati ambapo hakuna
taifa lolote ambalo halijaathirika na COVID-19 katika uchumi na mapato
yake".
"Ni muhimu kwamba wamegusia ukweli juu ya kiwango cha sasa cha vurugu kisichokubalika kabisa, na kutakuwa na usitishaji mapigano mara moja. Ni ujumbe mzito kwa Taliban kwamba sio tu watu wa Afghanistan ambao wanadai mapigano kusitishwa mara moja, sasa", alisema Atmar.
EmoticonEmoticon