Wanajihad Wawakata Vichwa Watu 50 Msumbiji

 

Takriban watu 50 wamekatwa vichwa na wapiganaji wa Kiislamu nchini Msumbiji, vyombo vya habari vya serikali vimeripoti.

Wapiganaji hao waliugeuza uwanja wa kuchezea kandanda kuwa 'kichinjio' , ambapo walikatakata miili ripoti nyengine zinasema.

Watu kadhaa pia walikatwa vichwa katika kijiji chengine , vyombo vingine vya habari viliripoti.

Uchinjaji huo ndio tukio la hivi karibuni katika msururu wa mashambulizi ya kutisha ambayo yametekelezwa na wapiganaji hao katika eneo lenye utajiri mkubwa wa gesi la mkoa wa Cabo - Delgado tangu 2017. Hadi takriban watu 2000 wameuawa na takriban 430,000 wengine wamewachwa bila makao katika mzozo huo katika mkoa huo ulio na Waislamu wengi.

Wapiganaji hao wanahusishwa na kundi la Islamic State , ambalo limeingia kusini mwa Afrika. Kundi hilo limetumia sababu ya umasikini na ukosefu wa ajira kuwasajili vijana wengi katika vita vyao vya kutaka kuwa na utawala wa Kiislamu katika eneo hilo.

Wakaazi wengi wanalalama kwamba wamefaidika kidogo na madini pamoja na viwanda vya gesi vilivyopo katika eneo hilo.

Credit:Bbc


EmoticonEmoticon