Watu 16 Wamekufa, 65 Kujeruhiwa, Zaidi ya 350 Wamekamatwa Uganda

Polisi nchini Uganda wamesema kwamba watu 16 wamefariki na 65 kujeruhiwa kufuatia vurugu zilizotokea baada ya kukamatwa kwa mgombea wa urais Robert Kyagulanyi maarufu Bobi wine.

Msemaji wa polisi jijini Kampala Patrick Onyango amesema kwamba zaidi ya watu 350 wamekamatwa.

Viongozi wa chama cha Bobi Wine wamesema kwamba polisi wamekataa mtu yeyote kuonana naye anapozuiliwa katika kituo cha polisi cha Nalufenya mjini Jinja, mashariki mwa Uganda.

Credit : DW


EmoticonEmoticon