Waziri mkuu
wa zamani wa Sudan, Sadiq al-Mahdi amefariki dunia kutokana na virusi
vya corona, mwanasiasa huyo amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika
nchi ya Umoja wa Falme za Kiarabu.
Mahdi aliyefariki akiwa na
umri wa miaka 84, ndiye Waziri Mkuu wa mwisho wa Sudan kuchaguliwa kidemokrasia
kabla ya kuondolewa madarakani mwaka 1989 kwa mapinduzi ya kijeshi
yaliyomuingiza mamlakani rais wa zamani Omar al-Bashir.
Chama chake cha Umma chenye siasa za wastani, kilikuwa moja ya vyama vikubwa vya upinzani na Mahdi alisalia kuwa kiongozi mwenye ushawishi.
EmoticonEmoticon