Waziri Mkuu Wa Ethiopia Asema Eneo La Magharibi Katika Jimbo La Tigray Liko Huru Sasa

 

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed amesema jeshi la Ethiopia limewashinda wanajeshi wa jimbo la Tigray huku akiwatuhumu wanajeshi hao kwa uhaini wakati wa mapigano yaliyodumu kwa wiki moja sasa na kutishia kuiyumbisha nchi hiyo ya Pembe ya Afrika. 

Katika ujumbe aliouandika katika mtandao wa kijamii wa Twitter, Abiy amesema eneo la magharibi mwa Tigray liko huru sasa, kwa sasa jeshi linatoa misaada ya kiutu na kuwapa watu chakula. 

Lakini huku ikiwa hakuna mawasiliano, usafiri ukiwa umezuiliwa na vyombo vya habari kuzuiwa kuingia eneo hilo na kuripoti, imekuwa vigumu kuthibitisha hali ya mzozo huo kwa sasa. 

Abiy anakituhumu chama tawala katika jimbo la Tigray TPLF kwa kuanzisha mzozo huo baada ya kuishambulia kambi ya jeshi na kuupinga uongozi wake, lakini chama hicho kinasema jimbo hilo limepitia mateso katika miaka miwili ya uongozi wa Waziri Mkuu Abiy.


EmoticonEmoticon